Skip to main content
x

Mamia ya wakazi wa Jiji la Dar es Salaam hii leo Jumatano Agosti 14, wamejitokeza kwa wingi ili kuungana na Benki ya Exim Tanzania ambayo kwa kusirikiana na Mpango wa Taifa wa Damu Salam (NBTS) waliendesha zoezi la uchangiaji damu kwaajili ya kusaidia majeruhi wa ajali ya moto iliyosababishwa na lori la mafuta lililopinduka na kulipuka eneo la Msamvu Mkoani Morogoro ambapo watu zaidi ya 70 walifariki dunia na wengine kujeruhiwa.

Zoezi hilo litakalodumu kwa siku tatu mfululizo limefanyika kwenye viunga vya Stendi ya mabasi ya Mbagala jijini Dar es Salaam ambapo imeshuhudiwa idadi kubwa ya wakazi wa eneo hilo wakijitokeza kwa wingi ili kujitolea damu huku wadai kuwa muitikio huo umetokana na kuguswa kwao na tukio hilo la kusikitisha lililotokea mkoani Morogoro.